Ruka hadi maudhui

Kazi

Bidhaa tulizosanifu na kujenga.

Kila moja ilianza kama swali mtu alituletea. Saba zinatumika leo; moja inajengwa.

Piku

Inatumika

Soko la Kitanzania ambapo watu hushinda bidhaa, kuanzia simu hadi safari, kwa zabuni ya chini isiyorudiwa. Imepewa leseni na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Jukwaa
Android

Panda Safiri

Inatumika

Panga safari ya kila siku, kata kiti na fuatilia basi popote Dar es Salaam. Imejengwa kwa ajili ya Taksibus, wanaoendesha huduma hii.

Faida

Inatumika

Mfumo wa mauzo wa kompyuta unaoendelea kufanya kazi intaneti ikikatika: mauzo, ankara, stoo, manunuzi na ripoti, vinavyosawazishwa mtandao ukirudi.

Jukwaa
Windows na macOS

Adili

Inatumika

Wanachama, mikopo, michango na idhini sehemu moja, pamoja na ripoti za TCDC na Benki Kuu ya Tanzania tayari kupakuliwa.

digid

Inatumika

Inasoma kadi ya NIDA, inalinganisha uso na kuchukua alama za vidole kwenye simu ya mteja mwenyewe, kwa modeli ndogo zinazoendeshwa ndani ya kifaa. Hakuna kinachohifadhiwa. SDK za Android, iOS, Flutter na mtandao.

Jukwaa
Android, iOS, Flutter na mtandao

Drafti

Inatumika

Cheza drafti kwa sheria za Kitanzania na watu wa Tanzania na duniani kote: mechi zenye viwango za bullet, blitz na rapid, ligi za vilabu, mashindano na fainali mubashara.

SolarFinanced Africa

Inatumika

Wawekezaji, waendelezaji na biashara hufuatilia miradi ya nishati ya jua, ufadhili wake na taasisi zilizo nyuma yake kote Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

Finvoice

Inajengwa

Biashara na wasambazaji wao hulipwa mapema kwa ankara ambazo tayari wamezitoa, na nyaraka zikiwa kwenye mpangilio.